MOROGORO PRESS CLUB
CHAMA cha waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro (Morogoro Press Club) mchakato wa kuanzishwa mwaka 1996 ilipofika tarehe 13/3/1997 ikapata usajili Wizara ya Mambo ya ndani na kupata cheti cha usajili chenye namba. SO.NO.9009 ikiwa na wanachama 20 kwa sasa Morogoro Press Club ina wanachama 100.
Ofisi ya MOROPC ipo katika jengo la Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Kata ya Kingo mkabala ya Mahakama ya mwanzo ya Nunge,Manispaa ya Morogoro.
MADHUMUNI NA MALENGO
1. Ni chama cha kitaaluma malengo yake mahususi ni kujenga mahusiano miongoni mwa wanachama na makundi yenye makusudio tofauti ikiwa ni pamoja na taasisi za raia.
2. Kuwa kitovu cha masuala ya waandishi wa habari katika mkoa wa Morogoro.
3. Kuhakikisha kuwa wanachama wake wanafanyakazi kulingana na maadili ya waandishi wa habari kama ilivyofafanuliwa na Baraza la Habari.
4. Kuinua kiwango cha taaluma katika tasnia ya habari kwa kuendesha mafunzo mafupi mafupi kwa wanachama wake.
5. Kuwezesha wanachama kutumia rasilimali chache zilizopo katika kuboresha shughuli za ukusanyaji na usambazaji wa habari miongoni mwa waandishi wa Watanzania.
6. Kuimarisha ushirikiano miongoni mwa waandishi wa habari,watoa habari na taasisi za kitaaluma zenye kulenga kuongeza ufanisi katika habari na mawasiliano kwa maanufaa ya wanachama wote na jamii na kuitangaza vema Mkoa wa Morogoro ili kusukuma maendeleo ya wananchi kwa kasi.
7. Kuwalinda waandishi wa habari dhidi ya madai yenye mwelekeo wa kitaaluma.
DHAMIRA:"Kuwaimarisha waandishi wa habari Kitaaluma"
DIRA:"Kuwa na jamii yenye uhuru wa kujieleza na Uhuru wa Habari"